Jeshi la polisi kanda maalumu ya Dar es salaam limepiga marufuku ngoma
za kitamaduni ambazo zimekuwa zikifanyika nyakati za usiku kwenye
maeneo mbalimbali Dar es salaam ikiwa ni muendelezo wa kukabiliana
makundi ya kihalifu ambayo yamekua tishio kwa usalama wa raia.
Kufuatia kuibuka kwa makundi ya kihalifu kama Panya road na Mbwa mwitu
ambayo wengi wao wanahusishwa na ngoma hiyo kwenye uporaji na upigaji wa
watu, Kamanda wa polisi kanda maalumu ya Dar es salaam Suleiman Kova
anasema ‘ni marufuku kwa ngoma yeyote ya asili kuchezwa nyakati za
usiku’
Kamanda Kova anasema kufuatia operesheni inayoendeshwa dhidi ya vikundi
hivyo vya kihalifu, mpaka sasa tayari wanawashikilia wafuasi zaidi ya
mia moja ambapo pia watu wengi wamekuwa wakilalamikia vitendo viovu
vinavyofanyika nyakati za usiku wakati wa ngoma hizo maarufu kama
‘vigodoro’ pamoja ‘baikoko’ na sasa jeshi la polisi limetoa onyo kali
kwa watakaoendeleza hizi ngoma kuanzia sasa.
Sign up here with your email
ConversionConversion EmoticonEmoticon