a

HATARII- - POMBE YAUA WATU 70 KENYA

Jumatatu asubuhi. Pombe hiyo iliyopewa jina la ‘Countryman’, inasemekana iliwekwa sumu aina ya Methanol na kusababisha baadhi ya waliokuwa wamekwenda kuibugia kufariki huku wengine wakisalia hali mahututi na wengine kupoteza uwezo wao wa kuona.

pombeWashukiwa waliouza pombe hiyo wameripotiwa kukamatwa
Madaktari wanafanya kila wawezalo kujaribu kuokoa baadhi ya waathiriwa ambao wamelazwa hospitalini.
Vifo hivyo vilianza kutokea mapema wiki hii katika mkoa wa kati na katika eneo la Mashariki mwa Kenya.
Inaarifiwa wengine wengi wamelazwa hospitalini baada ya kubugia pombe hiyo.
Idadi ya vifo ilianza kuongezeka huku watu wengine 14 wakifariki katika jimbo la Embu Mashariki mwa nchi , wengine wanne wakifariki katika jimbo la Makueni. Watu 75 wamelazwa hospitalini katika jimbo hilo wengine watatu wakiripotiwa kupoteza uwezo wao wa kuona.
Kwa sasa wataalamu wanafanyia utafiti kinywaji hicho pamoja na mkojo kutoka kwa wagonjwa kubaini kilichowekwa ndani ya pombe hiyo.
Matokeo yanatarajiwa katika siku mbili zijazo.
Previous
Next Post »