Mambo bado mabaya! Ule ugomvi wa
mashosti wawili nyota katika tasnia ya sinema Bongo, Wema Isaac Sepetu
‘Madam’ na Kajala Masanja ‘K’, sasa umechanja mbuga hadi kufika
mjengoni, ambako inadaiwa kuwa baadhi ya wabunge wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, wameingilia kati ili kuumaliza, Risasi Jumatano
linakuhabarisha.
Kwa mujibu wa chanzo makini, baada ya mvutano wao wa muda mrefu, wabunge hao walimwita Mwenyekiti wa Bongo Movie Unity, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ na kumuuliza kama ni kweli wawili hao hawaelewani.
Inadaiwa kuwa Steve alikiri kutokuwepo kwa maelewano kati ya wawili hao ambao awali walikuwa ni marafiki pete na kidole.
Ilisemekana kwamba baada ya kuhakikishiwa kuwepo kwa ishu hiyo, baadhi ya wabunge hao, hasa wapenda michezo na sanaa, walimuagiza Steve kulifanyia kazi tatizo hilo haraka, akishindwa basi awapelekee ili wawakalishe chini.
Gazeti hili liliwasiliana na Steve juu ya ukweli wa madai hayo, ambaye alikubali kuwa ni kweli baadhi ya wabunge wamemtaka kumaliza bifu kati ya waigizaji hao maarufu Bongo kwani nyuma yao kuna vijana wengi wanatamani kuwa kama wao.
Risasi Jumatano lilizungumza na mbunge wa Kinondoni Idd Azan ambaye alisema hata yeye atawaunga mkono wabunge watakaojitolea kuwasuluhisha mastaa hao.
Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ na Kajala Masanja ‘K’, wakiwa kwenye pozi enzi za ushosti wao.
Kwa mujibu wa chanzo makini, baada ya mvutano wao wa muda mrefu, wabunge hao walimwita Mwenyekiti wa Bongo Movie Unity, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ na kumuuliza kama ni kweli wawili hao hawaelewani.
Inadaiwa kuwa Steve alikiri kutokuwepo kwa maelewano kati ya wawili hao ambao awali walikuwa ni marafiki pete na kidole.
Ilisemekana kwamba baada ya kuhakikishiwa kuwepo kwa ishu hiyo, baadhi ya wabunge hao, hasa wapenda michezo na sanaa, walimuagiza Steve kulifanyia kazi tatizo hilo haraka, akishindwa basi awapelekee ili wawakalishe chini.
Wema Isaac Sepetu ‘Madam’.
“Walimwambia Steve kwamba ni kitendo cha
aibu kwa mastaa wakubwa kama hao kugombana, hiyo inawapunguzia heshima
kwani hiki kilikuwa ni kipindi cha kushikamana kwa umoja ili kuisogeza
mbele tasnia yao badala ya kulumbana,” kilisema chanzo hicho kikikataa
kutaja majina ya wabunge hao na kutaka aulizwe Steve.Gazeti hili liliwasiliana na Steve juu ya ukweli wa madai hayo, ambaye alikubali kuwa ni kweli baadhi ya wabunge wamemtaka kumaliza bifu kati ya waigizaji hao maarufu Bongo kwani nyuma yao kuna vijana wengi wanatamani kuwa kama wao.
Kajala Masanja.
Risasi Jumatano lilizungumza na mbunge wa Kinondoni Idd Azan ambaye alisema hata yeye atawaunga mkono wabunge watakaojitolea kuwasuluhisha mastaa hao.
Sign up here with your email
ConversionConversion EmoticonEmoticon