MKALI wa sinema za Kibongo, Lulu Semagongo ‘Aunt
Lulu’ amefunguka kuwa anasikitika kukosa bwana aliyeahidiwa na marehemu
Amina Ngaluma.
Akizungumza na paparazi wetu, Aunt Lulu alisema kabla marehemu Amina hajapatwa na mauti nchini Thailand, alimuahidi kumtafutia bwana nchini humo lakini mauti yalimkuta kabla hajamtimizia ahadi hiyo.
“We acha tu, aliniahidi
kunitafutia mume baada ya kugundua nasumbuliwa na wanaume kila wakati
lakini ndiyo hivyo tena Mungu akamchukua kabla hajanitimizia ahadi,” alisema Aunt Lulu.
Amina alifariki mwezi uliopita nchini humo ambapo chanzo cha kifo chake kikielezwa kuwa ni uvimbe kwenye kichwa.
Akizungumza na paparazi wetu, Aunt Lulu alisema kabla marehemu Amina hajapatwa na mauti nchini Thailand, alimuahidi kumtafutia bwana nchini humo lakini mauti yalimkuta kabla hajamtimizia ahadi hiyo.
Muigizaji wa sinema za Kibongo, Lulu Semagongo ‘Aunt Lulu’.
Marehemu Amina Ngaluma Enzi za uhai wake.
Sign up here with your email
ConversionConversion EmoticonEmoticon