a

IVORY COAST YAANZA VYEMA KOMBE LA DUNIA

Ivory Coast jana iliamsha matumaini ya Waafrika kwenye kombe la dunia linaloendelea nchini Brazil baada ya kuichapa Japan mabao 2-1 katika mchezo wa kundi C.
Magoli ya Ivory Coast yalifungwa na Wilfried Bony na Gervinho huku bao Japan likifungwa na Keisuke Honda. Kufuatia ushindi huo, kocha Ivory Coast Sabri Lamouchi amewataka wachezaji wake kutobweteka.”Wachezaji wamefurahi sana kutokana na ushindi huo, lakini bado tupo mbali sana na kufuzu,” alisema Lamouchi.
“Tumeshinda mechi moja tu. Bado tuna mchezo mgumu mbele yetu dhidi ya wanaongoza kwenye kundi [Colombia]. Tunahitaji kujiandaa.”
Previous
Next Post »