Kili Music Award 2015?
Msimu wa utoaji tuzo kwa wasanii wa muziki Tanzania wanaofanya
vizuri umewadia huku mchakato wa awali wa mchanganuo wa tuzo hizo za
Kili Tanzania Music Awards 2015 (KTMA) ukianza rasmi wiki hii.
Wakati mchakato huo ukisubiri mashabiki kuamua
msanii yupi aingie katika kipengele kipi, wasanii wengi watakuwa matumbo
joto kwa kile kinachoelezwa kwamba KTMA sasa zimekubalika zaidi kwao na
mashabiki wa muziki.
Hata hivyo, msimu huo unatojawa kuwa wenye neema
kwa wasanii, unazua maswali mengi vichwani mwa wasanii na mashabiki wao
moja likiwa; ni nani atavunja rekodi iliyowekwa na mwanamuziki Diamond
Platnumz mwaka jana?
Mbali na Diamond kuvunja rekodi msimu uliopita,
Bendi ya muziki wa dansi ya Mashujaa pia iliwahi kunyakua tuzo tano
mwaka 2013, huku wasanii, Kala Jeremiah na Ommy Dimpoz wakinyakua tuzo
tatu kila mmoja.
Shabiki wa muziki wa kizazi kipya na
mfanyabiashara katika Soko la Kariakoo, Omary Shaban alisema ushindani
kwa mwaka huu utakuwa mkubwa kwa tuzo hizo, hasa ikizingatiwa uwepo wa
wanamuziki wengi wazuri waliofanya kazi tofauti, zenye ubora na viwango
vya juu.
“Mwaka jana Diamond Platnumz alinyakua tuzo nyingi
kwa kuwa alijaribu kufanya kitu tofauti, lakini alichokifanya na
wengine wamefanya. Hivyo, ana ushindani mkubwa, pia Alikiba ambaye
alikuwa kimya amerudi. Hawa wawili ni washindani wakubwa, hivyo video
zao zitalumbana sana, yaani tunasubiri kumjua mkali nani,” anasema
Shaban.
Mshabiki mwingine, Ally Elly wa Dar es Salaam
alisema ni vyema kusiwepo ubabaishaji ili wapatikane washindani na
washindi halisi wa tuzo hizo kwa mwaka huu.
Mchakato utakavyokuwa
Waandaji wa mashindani hayo walisema kuwa kwa
mwaka huu kuna ongezeko la baadhi ya mambo, lengo likiwa ni kuboresha
utoaji wa tuzo hizo na kuwapa fursa Watanzania kupendekeza wasanii
watakaowania tuzo hizo kwa kuwapigia kura waingie kwenye kinyang’anyiro
kwa njia tatu kuu.
“Tumekuwa na juhudi za makusudi za kutenga fungu
kubwa na kuongeza ushiriki wa wataalamu kwenye fani husika ili
kuziendeleza, kuzikuza na kuziongezea thamani na umaarufu wa tuzo hizi
kimataifa mwaka hadi mwaka,” alisema Meneja wa Bia ya Kilimanjaro,
Pamela Kikuli. Bia hiyo ndiyo wadhamini wakuu wa tuzo hizo
“Wananchi watapata fursa ya kupiga kura
kupendekeza wasanii katika vipengele mbalimbali kwa kutumia njia tatu;
kwa mfumo wa website ya www.ktma.co.tz, mfumo wa mtandao wa WhatsApp na
kwa njia ya SMS.”
Alisema katika WhatsApp, mpigakura ataweza kutumia
namba ya simu na SMS kwa kutuma ujumbe wa neno KTMA au KILI na kisha
kufuata maelekezo kwa ajili ya kukamilisha zoezi hilo litakaloanza rasmi
Machi 30 hadi Aprili 19, mwaka huu litakapositishwa.
Kwa mujibu wa waandaji, baada ya upigaji wa kura kutakuwa pia na michakato mwingine wa kuwatafuta washindi, mpaka mwisho wa utoaji wa tuzo hizo ikiwamo kuchuja wapendekezwa kabla ya kuwarudisha tena kwa wananchi na kupigiwa kura za ushindi kuanzia Mei Mosi.
Kwa mujibu wa waandaji, baada ya upigaji wa kura kutakuwa pia na michakato mwingine wa kuwatafuta washindi, mpaka mwisho wa utoaji wa tuzo hizo ikiwamo kuchuja wapendekezwa kabla ya kuwarudisha tena kwa wananchi na kupigiwa kura za ushindi kuanzia Mei Mosi.
Sign up here with your email
ConversionConversion EmoticonEmoticon