Walimu watishia kuvuruga Kura ya Maoni
Rais wa chama cha walimu Tanzania (CWT), Gratian Mukoba, akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, kuhusu msimamo wa chama hicho kuunga mkono na kushiriki mgomo uliotishwa na Shirikisho la Wafanyakazi Tanzania(TUCTA, baada ya serikli kushindwa kuteleleza madai ya wafanyakazi.Picha na Michael Jamson
Dar es Salaam. Rais Jakaya Kikwete ametangaza
Aprili 30 kuwa ni siku ya kupiga Kura ya Maoni, lakini Chama cha Walimu
Tanzania (CWT) kinataka kuitumia kwa malengo tofauti; imepanga kuanza
mgomo nchi nzima wa kudai stahiki zao.
Chama hicho, ambacho kinaongoza walimu shule za
msingiu na sekondari wapatao 206,000 kwa mujibu wa takwimu za mwaka
2010, kimeeleza kuwa iwapo Serikali itakuwa haijatekeleza maazimio yao
matano ifikapo tarehe hiyo, walimu watachukua uamuzi mgumu kama ule wa
mwaka 2012.
Uamuzi huo uliofikiwa kwenye mkutano wa Baraza la
CWT uliomalizika Morogoro wiki mbili zilizopita, umekuja katika kipindi
ambacho wadau wengi wana shaka na utayari wa Serikali kufanikisha
mchakato wa Kura ya Maoni kutokana na viashiria vingi vya vikwazo, hasa
muda wa kutosha kutekeleza masuala yote yanayohitajika kama Sheria ya
Kura ya Maoni inavyotaka.
Ingawa Tume ya Uchaguzi (Nec) imeeleza kuwa mambo
yote yako sawa kufanikisha Kura ya Maoni, zikiwamo fedha za kuendeshea
mchakato huo, tamko hilo la CWT linaonekana litakuwa kizingiti kingine
kikubwa kwa Serikali, hasa kutokana na ukweli kuwa walimu ndio hutumika
sana kwenye shughuli za upigaji kura.
Akizungumza na gazeti hili jana, rais wa CWT,
Gratian Mukoba alitaja maazimio hayo kuwa ni kuitaka Serikali kulipa
Sh16 bilioni ambazo ni madeni ya walimu, kupandisha walimu wanaostahili,
kulipwa mishahara waliokuwa wanadai tangu mwaka 2012, mwalimu kuwa na
mwajiri mmoja kati ya Wizara ya Elimu na Tamisemi na kubadilishwa kwa
kanuni za viinua mgongo kwa wastaafu.
“Yote haya yanatakiwa kutekelezwa ifikapo Aprili
30 mwaka huu la sivyo Baraza litawataka walimu kuchukua uamuzi mgumu.
Fedha za kumlipa mwalimu zipo, lakini wanaozifaidi ni wachache,” alisema
Mukoba, ambaye pia ni rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi
Tanzania (Tucta).
“Ukisikiliza mijadala bungeni ni wizi na ufisadi.
Mara mishahara hewa... mara (sakata la uchotwaji fedha kwenye Akaunti ya
Tegeta) Escrow, lakini walimu hawalipwi wala kutatuliwa matatizo yao.
Hii ni kwa sababu Serikali iliyopo imeshindwa na umefika wakati sasa
kuiondoa madarakani.”
Mwaka 2012 CWT ilitikisa nchi baada ya kufanya
mgomo nchi nzima ulioungwa mkono na walimu wa shule za msingi, sekondari
na vyuo na ambao ulisambaa hadi kwa wanafunzi walioamua kuandamana ili
kuishinikiza Serikali kuwalipa walimu wao.
Mwaka huo, Julai 27 CWT iliandika notisi ya saa 48
kuhusu mgomo huo, lakini Serikali ikautangaza kuwa si halali kwa
maelezo kuwa unakiuka taratibu za kimahakama baada ya pande hizo mbili
kufikishana Mahakama Kuu, Divisheni ya Kazi kujaribu kutatua tatizo
hilo.
Jana, Naibu Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali
za Mitaa (Tamisemi) anayeshughulikia Elimu, Kassim Majaliwa alisema
hawajayapokea maazimio hayo.
“Wao wamefikia maazimio hayo, lakini sisi bado
hatujayapata na kama tukiyapata tutawaita na tutazungumza nao,” alisema
Waziri Majaliwa
“Mfano suala la madeni wao watakuwa wamelizungumza
kwa ujumla hivyo tukikutana tutaweza kuwaeleza tumefikia wapi katika
utekelezaji wa kila eneo.”
(from mwananchi website)
Lakini Mukoba alipofuatwa kuzungumzia kauli hiyo ya Waziri
Majaliwa, alisema: “Kama anasema hawajayapata, basi wasubiri Aprili 30
kuyapata. Serikali ina ubabaishaji na kama ndiyo hivyo mwambie asubiri
Aprili 30 atayapata maazimio hayo.”
Aliongeza kusema:”Kama anasema hawajui mbona
watumishi kutoka Tamisemi walikuwa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke
jijini Dar es Salaam wanafuatilia madeni ya walimu kama hawajui
wanachokifuatilia huko ni nini, wasubiri wataona?”
Nec ilikuwa imependekeza kutumia wanajeshi katika
mchakato wa Kura ya Maoni, lakini pendekezo hilo limepingwa na wadau,
hasa wanasiasa na wanaharaka ambao wamesema matumizi ya chombo hicho cha
dola yatatisha wananchi kujitokeza kujiandikisha kupiga kura na pia
siku ya kuhitimisha mchakato huo ambayo ni Aprili 30.
Kwa hali hiyo, Nec italazimika kutumia walimu
kwenye mchakato huo mkubwa na unaohitaji nguvu kazi kubwa hasa wakati wa
upigaji kura.
Tayari vyama vya upinzani vinavyoundwa Umoja wa
Katiba ya Wananchi (Ukawa) vimetangaza kujitoa kwenye mchakato huo wa
Kura ya Maoni, ambao utahusisha uandikishaji wa wananchi kwenye Daftari
la Wapigakura, utoaji wa elimu kuhusu yaliyomo kwenye Katiba
Inayopendekezwa, upigaji wa kampeni za kutaka wananchi waikubali au
waikatae na kuhitimishwa kwa kupiga kura.
Mchakato wa Kura ya Maoni imekuwa na vikwazo vingi
tangu wakati wa Bunge Maalum la Katiba wakati vyama vya upinzani
vilipodai kuwa chombo hicho kilikuwa kinapoteza mwelekeo kwa kuacha
kujadili Rasimu ya Katiba iliyowasilishwa na iliyokuwa Tume ya
Mabadiliko ya Katiba, na badala yake kujadili rasimu iliyokuwa na utashi
wa CCM.
Baadaye vyama hivyo vikaunda Ukawa na mwezi Aprili
vikasusia vikao vya Bunge la Katiba, na juhudi za kuwarejesha bungeni
zilkishindikanaSign up here with your email
ConversionConversion EmoticonEmoticon