Zaidi-ya wanafundi 50,000 watashindwa kuendelea na masomo ya elimu ya
juu kutokana na kushindwa kupata mikopo kutoka katika Bodi ya Mikopo ya
Elimu ya Juu (HESLB).
Hayo yamebainika ikiwa ni siku tatu tangu HESLB kutoa majina ya
wanafunzi waliofanikiwa kupata mikopo kwa mwaka wa masomo 2015/2016,
huku idadi kubwa ikiwa haimo katika majina hayo.Katika mwaka huu wa
masomo bodi ya mikopo imeweza kuwapatia mikopo wanafunzi 12,000 pekee
sawa na 17.1% ya waombaji zaidi ya 70,000, hivyo kufanya idadi ya
wanafunzi waliokosa mikopo kufikia asilimia 82.9 ya waombaji wote.
Wanafunzi waliokosa mikopo ya kuwawezesha kujiunga na elimu ya juu na
hivyo wazazi wao kutakiwa kugharamia elimu hiyo wameelezea kusikitishwa
na hali hiyo huku wakiitaka serikali kuwaangalia kwa jicho la kipekee
kwani hawana uwezo wa kuanza masomo pasipo kufadhiliwa na serikali.
Wanafunzi hao walionekana kukata tamaa ya kutimiza ndoto yao ya kujiunga
na elimu ya chuo kikuu, wamefika makao makuu ya bodi hiyo huku
wakiongozana na baadhi ya viongozi wa serikali ya wanafunzi kutoka Chuo
Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kutaka kujua hatima yao.
Nimetokea Tabora, wazazi wangu walinipa Sh. 100,000 ya kutumia wakiamini
tunapewa mikopo na serikali, lakini tumenyimwa na hatujui hatima yetu,
nimebakiwa na Sh. 6,000, naomba serikali ituhurumie, isikie kilio chetu
hatustahili kuteseka hivi,?-ameeleza Abdul Omary mwanafunzi mteule
UDSM.Fatuma Bakari, mwanafunzi mwingine kutoka UDSM, amesema:-
Siwezi kujiunga na Chuo bila mkopo, tumefika hapa ili kuomba bodi ya
mikopo itusaidie hatuna tumaini lolote zaidi ya kuomba Mungu atusaidie
tuweze kupata mikopo na kuanza masomo.
Waziri wa Mikopo serikali ya wanafunzi (Daruso), Shitindi Venance
ameeleza kutokukubaliana na majibu waliyopewa na uongozi wa juu wa bodi
ya mikopo kwani yanakatisha tamaa na kuzima ndoto za wanafunzi wa
masikini kusoma chuo kikuu.?Hapa UDSM ni wanafunzi 600 tu waliopata
mikopo kati ya wanafunzi 7,000 waliopangiwa kuanza masomo, hili ni janga
kubwa kwa watoto wa masikini kwani hawawezi kujisajili chuoni wala
kupata makazi katika mabweni mpaka walipe ada na wengi wametoka mikoani.
Tunachukua hatua moja mbele na kuamua kulifuatilia suala hili kwa katibu
mkuu wa wizara ya elimu na katibu mkuu wa wizara ya fedha kwa sababu
bodi bado wanasisitiza tuwe na subira ilihali muda umeenda na wanafunzi
wanateseka ameeleza Shitindi.
Mkurugenzi wa Habari, Elimu na Mawasiliano wa HESLB, Omega Ngole
amewaambia wanahabari waliofika ofisini kwake kuwa bodi haistahili
kulaumiwa kwani serikali kupitia wizara ya fedha na wizara ya elimu ndio
yenye uwezo wa kutenga kiasi cha fedha kulingana na mahitaji ya wakati
husika.
Lengo la bodi ya mikopo ni kuwawezesha wanafunzi wa vyuo vikuu kusoma
kwa ufadhili wa serikali na wala sio kuwakwamisha, tunaendelea
kujadiliana na serikali kuona kama itatuongeza fedha ili tuweze kutoa
awamu ya pili ya majina ya wanafunzi waliopata mikopo, tunawaomba
wanafunzi wavute subira,?-anaeleza NgoleHata hivyo Ngole amesema hawezi
kusema lini watatangaza majina ya awamu ya pili kwani hilo linategemea
ni lini serikali itatoa fedha kwa ajili ya wanafunzi wa awam ya pili.
Katika mwaka uliopita wa masomo 2014/2015 serikali ilitoa mikopo kwa
wanafunzi 30,000 sawa na 51.7% ya waombaji wote 58,000 na hivyo kufanya
waliokosa mikopo kuwa wanafunzi 28,000 sawa na 49% pekee tofauti na
mwaka huu ambapo waliokosa wamefikia asilimia 82.9
Chanzo: Mpekuzi blog
Sign up here with your email
ConversionConversion EmoticonEmoticon