a

Breaking News: Sheikh Issa Ponda Ashinda Kesi ya Uchochezi na Kuachiwa Huru


Mahakama ya hakimu mkazi Morogoro imemuachia huru Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Issa Ponda aliyekuwa akituhumiwa kwa makosa ya uchochezi baada ya mahakama kutoridhishwa na ushahidi wa upande wa mashtaka na hivyo kuonekana hana hatia

Makosa yaliyokuwa yakimkabili ni mawili ambayo ni kushawishi watu kutenda kosa, pamoja na kutoa matamshi yanayoumiza imani ya dini nyingine.

Hakimu wa kesi hiyo Mary Moyo amesema ushahidi uliotolewa na upande wa mashitaka haukujitosheleza hivyo mahakama hiyo imemwachia huru na rufaa iko wazi endapo upande wa mashitaka hautaridhika na hukumu hiyo.
Previous
Next Post »